Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Kufuatia tukio la kusikitisha la moto katika Bandari ya Shahid Rajaei mjini Bandar Abbas, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah Ali Khamenei, ametuma ujumbe wa rambirambi kwa familia za wahanga wa tukio hilo, sambamba na maagizo mahsusi kwa viongozi wa usalama na mahakama.
Katika ujumbe wake, Ayatollah Khamenei ameeleza huzuni na masikitiko yake kufuatia tukio hilo, na amewataka viongozi husika kuchunguza kwa kina tukio hilo, kubaini iwapo kulikuwa na uzembe au makusudi, na kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria.
Kiongozi huyo pia amesisitiza kuwa viongozi wote wanapaswa kujiona kuwa na wajibu wa kuhakikisha hatua madhubuti za kuzuia matukio kama haya zinachukuliwa.
Aidha, Ayatollah Khamenei amewaombea Marehemu rehma na msamaha kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na amewatakia familia za wahanga subira na utulivu wa moyo. Vilevile, amewaombea majeruhi wapate uponyaji wa haraka.
Katika ujumbe huo, ametoa shukrani za dhati kwa wananchi waliotoa damu kusaidia majeruhi katika kipindi cha dharura, akiwaita "watu wema na waungwana".
Mwisho wa Taarifa
(27 Aprili, 2025).
Your Comment